[Lyrics] Zuchu – Wana Lyrics






Lyrics
Hunywi Maji Yakapita me Nkiguna Ushafika
Jina Gani Hujaniita Baby
Ushauri Hutaki Kabisa eti Uniache Nna Visa
Vya Vifarauni Na Musa Vingi
Nikilala Naota Kama Unaniita
Nafumba Macho Navuta Shuka naona Napumbazika
Unishikapo Ndipo Hapo Nafarijika
Mambo Yako Mahaba Yako
Ndo Maana Natononoka Weee
Wana Wana Wana Wana pale Tulipokutana
Mikono Tukapeana macho Yakatizamana
Wana Wana Wana Wana pale Tulipokutana
Namba Kubadilishana nafsi Kukubaliana Aah!
Nzi Kidonda Nimefia wahenga Walisema
Maradhi Yaweza Yasiwe Na Dawa
Kwa Penzi Yakapona rabii Amenipa Nusura
Jeuri Sina Tena
We Ndo Ganzi Umenimaliza Hasira
Siumwi Wakisema nidekeze Niliwaze
Washushuke Wanyamaze nikuna Nibembeleze
Usinipepee Nipulize watuone Washituke
Roho Zao Ziwaume mi Nipike Ule Chote
Unenepe Upendeze
Wana Wana Wana Wana pale Tulipokutana
Mikono Tukapeana macho Yakatizamana
Wana Wana Wana Wana pale Tulipokutana
Namba Kubadilishana nafsi Kukubaliana Aah!
Ukitaka Uniweze Nibebe Wewe
Ukipenda Unibimbe Unikumbatie
Hata Watu Watuone Wakahadithie
Nitambulishe Niringe Niwavimbie
Ukitaka Uniweze Nibebe Wewe
Ukipenda Unibimbe Unikumbatie
Hata Lizer Atuone Akahadithie
Nitambulishe Nitambe Niwavimbie


Share [Lyrics] Zuchu – Wana Lyrics with others on social media;

Post a Comment

0 Comments